KANISA
la Moravian Jimbo la Mashariki limeitaka Serikali iangalie upya uamuzi
wake wa kuruhusu mgawanyiko wa kanisa hilo kwa kuruhusu usajili wa Jimbo
lingine ili kuepusha uvunjifu wa amani.
Na Zitto Kabwe,Mpekuzi. Katika ukurasa wangu wa facebook mnamo tarehe 25 Aprili 2015
niliandika kuhusu sababu za shilingi kuporomoka thamani na majawabu ya
namna ya kurejesha thamani halisi ya sarafu yetu.
WATU watano akiwemo dereva wa gari linalotumiwa na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, David Ligazio ,Novatus Ngope (47),
wamejeruhiwa vibaya na shambulio la kitu kinachodhaniwa ni bomu la
kutupwa na mkono kutoka kwa watu wawili wasiofahamika walipokuwa kwenye
sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani juzi.
WAKIMBIZI 800 kutoka nchini Burundi wameingia nchini kupitia mkoani
Kigoma huku wengine 87 wakirejeshwa nchini mwao baada ya kuingia nchini
kwa kupitia wilayani Ngara mkoani Kagera.