KATIKA hali isiyo ya kawaida, mkulima kutoka Kijiji cha Mjimtala
Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Eldoforce Bilohe (43) jana alitinga
makao makuu ya Chama Cha Mapindizi (CCM) kuchukua fomu ya kuomba ridhaa
kuteuliwa kuwa mgombea urais, bila kuwa na ada huku akiwa amebeba maji
ya chupa kwapani.
WAKATI Watanzania na hasa viongozi wa sekta binafsi, wakijiandaa
kupima uwezo na uelewa wa watangaza nia wa CCM, katika masuala muhimu ya
kiuchumi kwenye mdahalo ulioandaliwa kesho kutwa, chama hicho kimepiga
marufuku watangaza nia hao kushiriki midahalo hiyo.
WANAFUNZI
sita wa Sekondari ya CTC Kigonsera inayomilikiwa na Misheni ya Mbinga
mkoani Ruvuma na Mkuu wa Shule hiyo, Padre Yazint Kawonga, wamefariki
dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia bondeni kisha
kuwaka moto na kuiteketeza miili yao.
JESHI
la Polisi limefanikiwa kukamata Silaha, watuhumiwa wa uhalifu wa
kutukia silaha katika oparesheni iliyoendeshwa kwa nyakati tofauti
katika Jiji la Dar es Salaam.
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe,
ameibuka na kusema hajawahi kumshambulia kwenye mitandao Waziri Mkuu wa
zamani, Edward Lowassa kuhusu sakata la Richmond.