December 30 ilikuwa ni siku ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta kukutana na uongozi wa wizara ya habari, vijana, utamaduni, burudani na michezo Nape Nnauye.
Samatta na Mh Waziri wakiongea na waandishi wa habari
Mshambuliaji huyo ambaye anahusishwa kwenda kucheza soka la kulipwa katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji aliomba kukutana na waziri Nape ili kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa waziri wa wizara inayomuhusu na kuomba baraka kuelekea fainali ya tuzo za mchezaji bora wa Afrika zitazofanyika January 7 Abuja Nigeria. Video soon kwenye Ayo Tv mtu wangu
Dakika chache kabla ya kuongea na waandishi wa habari Samatta na Mh Napewakijadiliana na kushauriana
Shaffih Dauda wa Clouds Tv/Fm na wengine walikuwepo
Mh Nape akimuonesha Samatta sehemu ya kusaini wageni
Samatta akisaini kitabu cha wageni cha wizara ya michezo
Mbwana Samatta akiondoka ofisini kwa Waziri
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.