Uchunguzi wa siri uliofanywa na BBC umebainisha kuwa watoto wakimbizi wa Syria wamekuwa wakiajiriwa kinyume cha Sheria katika viwanda vya nguo nchini Uturuki.
Timu ya kipindi cha televisheni cha Panorama kinachorushwa na BBC kimebainisha kuwa vijana wadogo ambao hawana kibali cha kazi wamekuwa wakifanya kazi zaidi ya muda wa kawaida uliowekwa.
Mmoja wa vijana wadogo ana miaka kumi na mitano na hufanya kazi zaidi ya masaa 12 kwa kupiga pasi nguo kabla ya kusafirishwa kwenda Ulaya. Watoto hao wamekuwa wakitengeneza nguo zenye nembo za makampuni ya Uingereza na ile ya Spencer pia kwa ajili ya kampuni ya uuzaji nguo mtandaoni ya ASOS.
Wakosoaji wanasema kuwa makampuni hayo hayajafanya jitihada za kuondoa tatizo hilo lilioneshwa na Panorama.
Mwandishi wa kipindi cha Panorama Darragh MacIntyre amezungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Syria ambao wanaona kuwa wanafanyiwa unyonyaji katika maeneo yao ya kazi. MacIntyre amesema kuwa wameongelea kuhusu malipo madogo wanayopata na hali mbaya ya ufanyaji kazi, na wamesema kuwa wanajua kuwa wanafanyiwa unyonyaji lakini hawana cha kufanya juu ya hilo.
Mbali na kuwa na kanuni za maadili zinazomtaka msambazaji kutoa taarifa kama wanawatumia wafanyakazi walio chini ya umri wa miaka kumi na sita na kuwaweka kando ya eneo la uzalishaji, Makampuni yote yamesema hayatoweza kuvumilia unyonyaji au utumikwishwaji wa watoto kinyume na sheria.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.