Mchaka Zaidi

Monday, October 24, 2016

Mourinho kakubali kipigo cha 3 EPL dhidi ya Chelsea Stamford Bridge


Jumapili ya October 23 2016 ndio siku ambayo kocha wa Man United Jose Mourinho alirudi tena Stamford Bridge kwa mara nyingine kucheza dhidi ya timu yake ya zamani ya Chelsea
 akiwa kakaa upande wa timu za wageni, Mourinho safari hii alirudi Stamford Bridge akiwa kocha mkuu wa Man United baada ya kufukuzwa na Chelsea December 17 2015.
39a32a2e00000578-3864700-image-a-1_1477239572184
Kwa bahati mbaya licha ya Jose Mourinho kuwa na heshima kubwa katika klabu hiyo alikaribishwa kwa kushuhudia Man United ikifungwa kwa mara ya 51 na Chelsea, licha ya kuwa Man United ni wababe kwa rekodi kwa kuwahi kuwafunga Chelsea kwa mara 75, huku wakiwa wamesuluhu mara 49, wamekubali kipigo cha goli 4-0.
39a35be700000578-3864700-image-a-55_1477241423069
Kikosi cha Chelsea kilichokuwa chini ya kocha muitaliano Antonio Conte kiliiadhibu Man United kwa kuifunga goli 4-0 licha ya kuwa Man United waliutawala mchezo kwa asilmia 56 kwa 44, magoli ya Chelsea yalifungwa na Pedro Rodriguez dakika ya 1, Garry Cahilldakika ya 21, kipindi cha pili dakika ya 62 Eden Hazard akaua dalili za Man United kutafuta walau suluhu.
39a36c6d00000578-3864700-image-a-59_1477241519530
Goli la Ngolo Kante dakika ya 70 ndio lilifanya mashabiki wa Man United waanze kuondoka uwanjani wakiwa hawana matumaini tena ya kupata matokeo katika mchezo huo, Man United sasa anakuwa kafungwa mchezo wa  tatu wa EPL msimu huu katika mechi zake tisa alizocheza za Ligi Kuu England.

epla
Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa baada ya mechi za leo(jana) October 23 2016

CHANZO:millardayo.com

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.