Mchaka Zaidi

Wednesday, March 30, 2016

Tanzania shughuli tunayo June 4 na September 3

Siku zinazidi kusogea na matumaini ya Tanzania yanazidi kupungua kuhusu safari ya Gabon mwaka 2017 katika michuano ya mataifa ya Afrika. Baada ya timu ya taifa ya Chad kujiondoa katika michuano ya Mataifa ya Afrika na kuacha mtihani Kundi G lenye timu za TanzaniaMisri na Nigeria.

March 29 timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles iliondolewa na Misri katika mbio za kuwania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2017 itakayofanyika Gabon,Nigeria ilitolewa baada ya kufungwa goli 1-0 katika mchezo wa marudiano.
_88991537_egyptnigeria
Jitihada za Ramadan Sobhy kuifungia Misri goli dakika ya 66 ndio zilizoiondoa Nigeria kwani hawakufanikiwa kusawazisha,  Nigeria inaaga mashindano hayo na nafasi pekee inabakia kwa Tanzania na Misri, kwani Nigeria imebakiza mchezo mmoja dhidi yaTanzania na hata ikishinda haitaweza kusonga mbele.
raaaaaa
Msimamo wa Kundi G ulivyo kwa sasa
Kazi imebakia kwa Tanzania kushinda mechi zake mbili dhidi ya Misri June 4 uwanja wa Taifa na Nigeria September 3 utachezwa Nigeria, kama Tanzania itashinda mechi zote mbili kwa idadi kubwa ya magoli, itakuwa imeizidi Misri kwa tofauti ya magoli. Nigeria ikiifunga Tanzania itakuwa inatimiza point 5 pekee.

Source:millardayo.com

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.