Mchaka Zaidi

Tuesday, October 31, 2023

Ronaldo alinishawishi nijiunge na Al-Nassr -Telles

 


Mazungumzo ya Cristiano Ronaldo yalisaidia kumshawishi beki wa pembeni Mbrazil 

Alex Telles kuondoka Manchester United na kujiunga na nyota huyo wa Ureno katika klabu ya Al-Nassr kwenye Ligi Kuu ya Saudia.

Telles, ambaye alishinda Ligi ya Europa msimu uliopita akiwa kwa mkopo Sevilla, alisaini mkataba hadi 2025 na Al-Nassr mnamo Julai.

“Wakati Al-Nassr alipozungumza nami kwa mara ya kwanza, nilimtumia Cristiano massage na jibu lake lilikuwa ni kuja (kuungana naye),” Telles alisema katika mahojiano yaliyotumwa kwenye jukwaa la ujumbe X, ambalo zamani lilijulikana kama Twitter.

“Kwa kweli, Cristiano anaendelea kukuza na uzoefu wake unaongezeka kila siku.

“Angalia idadi ya mabao anayofunga. Nitakuwa na upendeleo nikimzungumzia kwa sababu ya rekodi alizovunja, na nilibahatika kucheza naye Manchester United na kisha Al-Nassr.

“(Ronaldo) bado ni mchezaji madhubuti na kiongozi mzuri ambaye huwa anawajibika katika chumba cha kubadilishia nguo, husaidia kila mtu na hutengeneza mazingira mazuri.”

Al-Nassr wanashika nafasi ya pili kwenye jedwali la ligi wakiwa na alama 25, wakiwa nyuma ya vinara Al-Hilal nne

Chanzo:Millardayo


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.