Mashabiki wa soka wa Tanzania ambao wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya soka la nahodha wao wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk ataifanyia nini katika mchezo wa kwanza wa UEFA Europa League hatua ya 16 bora dhidi ya KAA Gent kutoka Ubelgiji pia.
Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk walikuwa ugenini kucheza mchezo wao huo wa kwanza wa Europa League hatua ya 16 bora dhidi ya KAA Gent, Samatta anarudi katika historia tena baada ya kufanikiwa kuifungia goli mbili KRC Genk dhidi ya KAA Gent katika ushindi wa 5-2.
Mbwana Samatta anafunga goli hizo mbili katika mechi yake ya 9 ya Europa League toka waingie katika hatua ya makundi na alikuwa hajafunga goli lolote, magoli ya Genk yalifungwa na Ruslan Malinovsky dakika ya 21, Omar Colley dakika ya 33, Mbwana Samatta dakika ya 41 na 72 na Jere Uronen dakika ya 45.
KAA Gent ambao watalazimika kuifuata KRC Genk katika mchezo wa marudiano March 16 2017, magoli yao mawili yalifungwa na Samuel Kalu dakika ya 27 na Kalifa Coulibaly dakika ya 61, ushindi huo unawapa matumaini ya zaidi ya asilimiana 50 Genk kucheza robo fainali maana ili watolewe labda KAA Gent ashinde kwa goli 4-0 mchezo wa marudiano.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.