Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
amewaambia mawaziri wa Afrika Mashariki kwamba endapo atachaguliwa
kuiongoza nchi hiyo mwezi June mwaka huu kwa muhula wa tatu basi itakuwa
ni kipindi cha ukomo wa yeye kuendelea kusalia madarakani ,msemaji wa
serikali ya Burundi Gervais Abayehorwa amesema hayo mapema Jumatano.
MWENYEKITI
wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameieleza
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa, hawakufanya
maandamano wala kupata barua ya zuio badala yake alipigwa na polisi.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema
kuwa alipofukuzwa Uanachama katika chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) alitamani kujiunga na Chama Cha NCCR-Mageuzi kwani ndicho
chama ambacho kilikuwa kinaendana
na itikadi yake anayoifuata na kuiamini ambayo ni itikadi ya Ujamaa.
KANISA
la Moravian Jimbo la Mashariki limeitaka Serikali iangalie upya uamuzi
wake wa kuruhusu mgawanyiko wa kanisa hilo kwa kuruhusu usajili wa Jimbo
lingine ili kuepusha uvunjifu wa amani.