BAADA
ya watani zao wa jadi Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu vita ya kuwania
kushiriki michuano ya kimataifa sasa mwakani imesalia kwa vigogo wengine
wa soka nchini Simba SC na Azam FC.
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru Mbunge wa Jimbo la Bahi mkoani
Dodoma, Omary Badweli, aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ya
kuomba na kupokea rushwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga.
KIKAO cha viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), kimeshindwa kuendelea baada ya baadhi ya wajumbe kushindwa
kuafikiana kuhusu hoja iliyowasilishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi, ya
kutaka kujitoa kwenye umoja huo, imefahamika.
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewatoa hofu wanachama wake
mkoani Shinyanga kikidai propaganda zinazoenezwa na Kiongozi Mkuu wa
Chama cha ACT-Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe, anayedai chama hicho
kimepoteza mwelekeo si za kweli bali ni uongo.
Chama
kipya cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa zamani wa Jimbo la
Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (pichani juu), kimebadili jina lake la
awali la ACT-Tanzania.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais( Muungano) Samia Hassan Suluhu amesema
kero mbalimbali za Muungano zilizoibuliwa zimeanza kufanyiwa tathmini na
Serikali.