Mchaka Zaidi

Saturday, April 25, 2015

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Tarehe 25 April 2015



Polisi Anusurika Kuuawa na Wananchi Wenye Hasira Kali Mkoani Morogoro jana Mchana


Askari mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria, aliyejulikana kwa jina la Ramadhani, amenusurika  kuuawa  leo (jana)  mchana  na wananchi wenye hasira mjini Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya dereva wa bodaboda ambaye aliparamia lori.
 

Afande Sele: Nikichaguliwa Kuwa Mbunge Nitakataa Posho na Mishahara Mikubwa


Mwana hip hop na Bongo Fleva nchini, Afande Sele, ameweka wazi kwamba hata kama atakuwa mwakilishi wa wananchi katika bunge la mwakani, hataweza kuacha kufanya muziki kwa kuwa ndiyo njia ya kumuingizia kipato.
 

CCM Wamjibu Dr. Slaa Kuhusu NEC......Wakanusha Kukisaidia Chama Kipya Cha ACT-Wazalendo



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amekanusha madai yaliyotolewa na  Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kuandikisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika ngome za CCM na kueleza kuwa  huo ni upotoshaji mkubwa kwani Tanzania  nzima ni ngome ya chama hicho.

Wednesday, April 22, 2015

Breaking News: Watu 10 Wafariki Dunia Baada ya Basi la kampuni ya Unique Kugongana na Gari la Coca Cola



Habari  zilizotufikia  zinaarifu  kuwa  basi la Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora limegongana uso kwa uso na lori la kampuni la Cocacola katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga.

Mapambano Bado Yanaendelea......Jana CHADEMA na ACT-Wazalendo Nusura Wakutane Uso Kwa Uso Nyumbani Kwa Baba wa Taifa. Vurugu Za Mnyika Ziligonga Mwamba Kwa Mara Nyingine


Mtoto wa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Andrew Nyere, akiteta jambo na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na kuvaa kofia ya Chama cha ACT-Wazalendo wakati viongozi wa chama hicho walipofanya ziara kijijini Mwitongo Wilayani Butiama.

Mambo Yameiva: Mmiliki wa Gombe high School, Dkt Yared Fubusa Atangaza Nia Ya Kugombea Ubunge Jimbo La ZITTO KABWE Kwa Tiketi ya CHADEMA


Mwanzilishi na  Mkurugenzi wa Gombe school of Environment and Society (GOSESO) na mmiliki wa Gombe high school, Dkt Yared Fubusa ambaye pia ni kada wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ametangaza nia ya kugomba ubunge jimbo la Kigoma kaskazini kupitia chama hicho.